Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UN News

Makala Maalum

Msaada wa Kibinadamu Mratibu Mkuu wa Misaada ya Dharura wa Umoja wa Mataifa kwa kushirikiana na Kamishna Mkuu wa  Umoja wa Mataifa wa Wakimbizi wamezindua ombi la pamoja la msaada wa kibinadamu la jumla ya  dola bilioni 6, tarehe 17 February 2025, ambalo ni  ombi kubwa zaidi kuwahi kutolewa kwa ajili ya Sudan ili kusaidia takribani watu  milioni 21ndani ya Sudan,pamoja na hadi watu milioni 5 wengine, wengi wao wakiwa wakimbizi waliokimbilia nchi jirani.

Habari Nyinginezo

Amani na Usalama Nchini Sudan Kusini, matumaini mapya yamechipua baada ya watoto waliokuwa wametumikishwa kwenye jeshi la nchi hiyo, SSPDF kuachiliwa rasmi katika hafla iliyoungwa mkono na Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, UNMISS. Tukio hilo limeelezwa kuwa ishara muhimu ya kumaliza utumikishaji wa watoto katika jeshi na kuwapa nafasi ya kujenga maisha mapya.   
Tabianchi na mazingira Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo (UNDP) nchini Tanzania limeelezea jinsi warsha mbili ilizoendesha katika mikoa ya Tanga na Mtwara kuhusu dhana ya uchumi rejeshi zimeanza kuzaa matunda kwani sekta hiyo ina fursa kubwa za kiuchumi, kiteknolojia, na kimazingira.